JINSI YA KUFLASH SIMU
TAHADHARI
1. Kuna uwezekano simu yako ikafa kabisa wakati unaifanyia upgrading au flashing.
2. Ni lazima kutumia file husika na sahihi la simu yako, kama ni Tecno Y6-Download file la Tecno Y6 na siyo la Tecno y3
3. Fuata kila hatua kwa usahihi kabisa, ukiruka step kuna uwezekano na simu yako nayo ikaruka!
4. Hatutahusika na uharibifu wowote wa simu yako, kwa hio kuwa mwangalifu na pia kumbuka kukosea ndio kujifunza.
5. NB; Hili somo ni general, kwa hio kama simu yako haitakubali, usisite kutuuliza kupitia mawasiliano HAYA HAPA!
MAHITAJI NA HATUA ZA AWALI
>>>Katika somo hili tutatumia App ya Rashr (Root) kubadili ROM ya simu husika.
>>>Lazima uwe ume Root simu yako, kama bado download King Root HAPA!, halafu fuata maelekezo ya jinsi ya ku root HAPA! kama huyajui! (NB; Siyo lazima utumie kingroot, tumia njia yoyote kuroot simu yako!)
>>>Download Rashr (Root) HAPA! halafu i Install kwenye simu yako!
>>>Download Custom Rom ya simu yako, Mfano Custom Rom for Tecno Y6. Unaweza kuzipata kwa kutafuta Google, au unaweza kuingia HAPA kupata ROMS mbalimbali za simu. Usilifungue hilo Zip file. NB; Download Android Version sahihi kwa simu yako, inaweza kuwa Mashmallow, Lollipop etc na UIWEKE MOJA KWA MOJA KWENYE MEMORY CARD na SIO ndani ya file kwenye memory Card!
>>>Download Recovery Image ya simu yako (Eg, Recovery Image for Tecno Y6) na iweke moja kwa moja kwenye Memory Card kama ilivyoelezwa hapo juu! Tafuta recovery image google au unaweza kutafuta HAPA!
>Ukishafika hapa, kunywa maji kidogo sababu kazi ndio inaanza!
HATUA ZA KUFLASH SIMU NA KUWEKA ROM MPYA!
MUHIMU; Rashr itatumika kufungulia Recovery Image, Recovery Image itatumia ku Factory Resest, ku Clear Cache, Ku Install hio ROM mpya na pia Kureboot!
1. Fungua Rashr, itakuomba root Access ikubali, inaweza pia kuomba kuinstall some Updates, we kubali tuu! Then chaguaRecovery From Storage then itafungua memory card, tafuta ile recovery image halafu lichague, ukishalichagua clickReboot in to recovery, au maneno mengine kama hayo, sababu Rashr zinatofautiana interface!
Rashr ikishafunguka iko hivi |
2. Ikishafunguka kwenye recovery mode utatumia Volume Up na Volume Down kuch agua unachotaka kufanya na kukubali (OK) utatumia Power Button (Cha Kuwashia simu).
FANYA VITU HIVI, chagua Wipe Cache, ikishamaliza rudi back na chagua Wipe Data (Kumbuka hii itafuta data zako zote kwenye simu, kwa hio ni vizuri kufanya Backup ya data zako, kama hujui jinsi ya kufanya hili, soma HAPA!)
3. Then chagua Install Zip from sd card na hapa chagua lile file lako (ROM) uliloliweka kwenye memory card katika hatua za awali.
Recovery mode |
Comments
Post a Comment